Matokeo ya mchakato wa elimu

Baada ya kukamilisha programu, inatarajiwa kuwa matokeo ya mchakato wa elimu yatakuwa yafuatayo:

  • Wawe wanafunzi ni wenye kufahamu kile wanachohitaji kutoka katika maarifa ya awali ya kisheria ambayo dini husimama kwayo.
  • Mwanafunzi ahakikishe matunda muhimu ya kutafuta elimu ambayo ni kumuabudu Allah kwa utambuzi na elimu.
  • Mwanafunzi anapaswa kuchangia kufundisha familia yake na jamaa zake kile wanachohitaji katika mambo ya dini yao,hali ya kuwa amejiweka mbali na msimamo mkali na kuchupa mipaka, na kwa njia inayowaongoza kwenye maadili mazuri na sifa nzuri.
  • Mwanafunzi anapaswa kujiendeleza kama anapenda elimu hii na na kuongeza Zaidi katika elimu hii hadi aweze kufanya kazi katika uwanja wa kumlingania Allah, na maeneo mengi ya huduma za kielimu kama vile utafiti wa kielimu ya sharia,au uchunguzi na ukaguzi, au kuandaa  utafiti wa kielimu, na kuandaa masomo, hotuba na mihadhara.
  • Programu hii inapaswa kumsaidia mwanafunzi kusomesha  na kutoa hotuba katika masuala ya kielimu anayoyaweza katika misikiti na maeneo ya umma, au kwenye mtandao, kama vile kuandika na kuchapisha makala za kisheria.
Hakika Allah yuko nyuma ya nia na yeye ndiye mwenye kuongoza katika njia ya haki.
×