Neno la msimamizi mkuu

Kila sifa njema anastahiki Allah mol mlezi wa viumbe vyote,sala na salamu ziwe juu ya yule aliyewafundisha watu mambo ya kheri (Muhammad S.A.W) pamoja na familia yake na maswahaba zakee wote,ama baada ya kusema hayo:

Hakika elimu ya sharia ndio njia itakayomfikisha mtu katika kupata radhi za Allah na kufuzu kwa kupata daraja za juu katika pepo, Na ndio elimu inayomfikisha mtu katika kheri zote za dunia na akhera,na mzunguko wa ubora wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla upo katika kuisoma elimu hii, Na kwa elimu hiyo jamii zinapata utukufu wake na kuongoza.

Na bora ya alama ambayo hujipamba nayo wanaosoma ni kauli ya Allah mtukufu aliposema: ((Allah huwanyanyua daraja wale walioamini miongoni mwenu na wale waliopewa elimu)) Al Mujadala:11

 ((Ameshuhudia Allah na malaika na wanazuoni kwamba hapana mola aabudiwae kwa haki ispokuwa yeye)) Al Imran:18.

Amesema Allah mtukufu: ((Na sema ewe Muhammad mola wangu mlezi nizidishie elimu)).

Na zimekuja dalili nyingi sana zikizungumzia ubora wa elimu na wale wanaosoma,amesema Mtume (S.A.W) (( Na yoyote atakayefuata njia ya kutafuta elimu;basi Allah humuwepesishia kwa njia hiyo njia ya kwenda peponi.)) Amepokea Muslim.

Kwa hiyo, (Africa Academy) ilikuja kama Academy ya kwanza ya kielektroniki/kimtandao iliyoelekezwa kwa jamii za Kiafrika kwa wale wasiozungumza lugha ya Kiarabu, ilikuja kukidhi haja ya Waislamu katika elimu ya Sharia ya Kiislamu katika bara la Afrika kwa lugha tofauti na kuwezesha kutafuta elimu kwa njia ya mtandao kwa wale wenye majukumu na wasio na majukumu.

Programu ya Academy inahusika na kujifunza elimu ya kisheria inayotokana na Qur’an na Sunnah sahihi, kwa ufahamu wa wema waliotangulia na itikadi yao, na mtaala umeanzishwa kwa uwiano na wanafunzi kwa kuzingatia utaratibu (kidogo kidogo), urahisi na ukamilifu ambao Muislamu anahitaji kutoka katika elimu ya dharura (msingi) na mbali na upanuzi wa tofauti za wanazuoni katika maswala ya kifiqhi, na imeundwa kwa njia bora za kiufundi na miundo ya kipekee zaidi ya kozi ili kuwezesha wanafunzi kupokea na kuendana na nyakati katika maendeleo yake ya utambuzi na mbinu za kisasa za elimu.

Ninamuomba Allah atuwafikishe, atuthibitishe na atunufaishe sote kutokana na yale yanayofundishwa na Academy na ninamuomba yeye mtukufu Ikhlas na kukubaliwa.

Sheikh Muharam Mwaita
×