Afrika Academy imeundwa kwa lengo la kusaidia jamii za Kiafrika katika uelewa sahihi wa Uislamu kupitia Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Ni jukwaa la kimtandao linalotoa programu ya elimu unaolenga kuleta elimu karibu na wale wanaovutiwa nayo, kupitia intaneti, mitandao ya kijamii na chaneli za Africa TV.
Jukwaa hili limetegemea mfumo wa kozi fupi katika kutoa elimu ya wazi. Ambayo kifupi hufahamika kama (MOOCs) Academy hii hufanya kazi kwa 100% kwa njia ya elektroniki, ambapo wanafunzi wanaweza kupata kozi kupitia kompyuta na simu janja (smart phones), kuhudhuria kozi kupitia mada za kuangalia (video), vitabu vya kieletroniki ambavyo mwanafunzi anaweza kuamiliana navyo na kujibu maswali ya tathmini.
Pia Africa Academy Swahili inategemea kada wa kipekee kabisa katika elimu ambao ni wahubiri (walinganiaji) maarufu wa Ahlu Sunnah wal-Jama’ah wanaozungumza lugha ya Kiswahili.
Tunatamani kuwa na wanafunzi 10,000 (elfu kumi) walionufaika kwa kujiunga nasi katika awamu tatu za kwanza za masomo.
Kuwa Academy inayoongoza katika kusomesha kwa njia ya mtandao kwa lugha ya Kiswahili kwa kutumia mbinu na njia za kisasa zaidi kama utangazaji kwenye vituo vya chaneli za televisheni na majukwaa mengine mbalimbali ya mtandao.