Stashahada (Diploma) ya masomo ya Sharia katika Afrika Academy inafundishwa katika mfumo wa kozi, ambapo kozi zinafundishwa mfululizo, ambapo wanafunzi husoma somo moja hadi wakamilishe pamoja na lulifanyia mtihani, na kisha kuendelea na somo linalofuata.
Video za mihadhara katika chaneli ya Africa TV
Mihadhara ya sauti (mp3)
Vitabu (pdf)
Matangazo ya moja kwa moja kwenye YouTube
Ni mitihani ambayo huwa mwishoni mwa kozi kwa lengo la kupima ufahamu wa wanafunzi na kutathmini uwezo wao, na ni mitihani ya lazima kwa kila kozi, ambayo muda wa kufanyika kwake huwa ni siku tatu.
Ni mitihani ya kufidia/marudio kwa wanafunzi ambao hawakufikia daraja la kufaulu katika mitihani ya msingi au hawakufaulu mitihani ya msingi.
Mitihani yote hii hutolewa kwa mara moja mwisho wa muhula – mtihani wa kufidia/marudio kwa kila kozi – na muda wake ni siku kumi.
Jumla ya alama kwa kila kozi ni 100
Alama ya kufaulu katika mitihani ya mwanzo au mitihani ya kufidia/marudio ni 50 au zaidi
Kwa kupata alama za ufaulu katika mihula miwili, mwanafunzi ana haki ya kupata cheti cha kidigitali kinachotolewa na Academy, ambacho anaweza kukisoma na kupakua kutoka ndani ya akaunti yake kwenye jukwaa.
Haki zote zimehifadhiwa © 2024