Jukwaa la Kiafrika la mtandaoni la kufundisha Elimu ya Kisheria bure kabisa.
Africa Academy ni akademi ya mtandao/kielektroniki inayotoa programu ya elimu kwa lengo la kuzisaidia jamii za Kiafrika kuwa na ufahamu sahihi wa Uislamu kwa kuzingatia ushahidi wa Qur’ani Tukufu na Sunnah za Mtume, kwa kutumia mtandao wa intaneti, mitandao ya kijamii. na luninga za chaneli za Afrika TV. Akademia hii inatokana na kada mashuhuri ya wanazuoni na mashekhe mashuhuri wa Ahlu Sunnah Wal-Jama’ah wanaozungumza lugha za Kiafrika.
Akademi inategemea mfumo wa masomo wa masafa (kupitia mtandao) , ambapo mwanafunzi anachagua njia ya kusomea ambayo inaendana nae zaidi miongoni mwa njia tofauti zinazopatikana.
Pakua faili la mwongozo wa mwanafunzi kufahamu mpango kamili wa masomo katika jukwaa
Video za mihadhara katika chaneli ya Africa TV
Mihadhara ya sauti (mp3)
Vitabu (pdf)
Matangazo ya moja kwa moja kwenye YouTube
Mwanafunzi anasoma katika somo la Aqidah: Maana ya Aqidah, na kuelezea njia ya Ahl al-Sunnah wal-Jama’ah katika itikadi kwa njia rahisi, isiyokuwa na makosa, pamoja na kusoma vyanzo vya kupokea elimu ya Aqidah, na kile kinachotofautisha itikadi ya Kiislamu, na maana ya Tauhidi na vigawanyo vyake, na maeneo ya kuteleza yaliyotokea ndani yake, na misingi ya tauhidi ya Uungu, na humpa mwanafunzi kinga ya kielimu ambayo ataweza kujibu shubha (hoja tata) mbalimbali kama vile shubha za wasioamini Allah, na za watetezi (walinganiaji) wa kurudia ufahamu upya wa maandiko ya kisheria, ufafanuzi juu ya kukufurisha na vidhibiti vyake, alama za Qiyama, Maswahaba na familia ya nyumba ya mtume, Allah awaridhie, mawalii na karama zao, maombezi, na uombezi, na mambo yanayohusiana nayo.
Mwanafunzi anajifunza yafuatayo katika somo la tafsiri: utangulizi wa elimu ya tafsiri, tafsiri ya surat Al-Fatihah, ayatul Kursiy, aya za mwisho wa surat Al-Baqarah, na tafsiri ya Juzuu ‘Amma yote, pamoja na kutaja faida muhimu zaidi za aya, na imetegemea katika maandalizi yake na uundaji juu ya vitabu muhimu na maarufu vya tafsiri za wanazuoni wa zamani na wa kisasa.
Katika somo la hadithi, mwanafunzi anasoma hadithi muhimu zaidi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilizochaguliwa, ambazo zinawakilisha misingi ya Sharia, misingi ya maadili, adabu na makatazo, zinayotokana na vitabu muhimu zaidi vilivyosherehesha Hadithi, Aqidah na adabu za kisheria.
Katika Fiqhi, mwanafunzi anasoma ibada ambazo Muislamu lazima ajifunze, kuanzia kwenye twahara na kuishia na Hijja, kisha kuishia na kitabu kilichokusanya shughuli za kifedha kwa njia fupi na rahisi, baadhi ya majanga ya kitabibu, masuala muhimu zaidi ya fiqhi ya familia, viapo na nadhiri, na masuala katika vinywaji na vyakula, kwa njia ya kisasa na ya ubunifu, na yote haya yanakuwa yameambatanishwa na picha, na uwasilishaji rahisi, ambao unategemea dalili kwa kiasi kikubwa, bila kuwepo maneno magumu na tofauti za ulamaa.
Mwanafunzi anasoma somo la sira ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwa ukamilifu, kwa namna fupi, kisha anasoma sifa za Mtume, kisha anajifunza kuhusu baadhi ya matukio na hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika maisha yake, na katika ngazi ya mwisho anasoma kwa ufupi katika miamala ya Mtume na makundi ya watu, kwa kutaja faida za maneno ya wanazuoni waliotangulia.
Katika elimu ya malezi yaKatika elimu ya malezi ya Kiislamu, mwanafunzi anasoma milango mbalimbali ya utamaduni wa Kiislamu, ambayo haihusiani na moja ya mitaala iliyopita, hivyo anasoma katika ngazi ya kwanza somo la haki, ikiwa ni pamoja na haki za Allah, kisha haki za Mtume, amani iwe juu yake, kisha haki za Maswahaba, kisha haki za wazazi, kisha haki za mume na mke. nk, na katika ngazi ya pili anajifunza matendo ya mioyo kwa ukamilifu, kuanzia Ikhlas, Tawwakkul, Subra na kuridhika. nk, kisha anasoma Adabu za Kiislamu, na kisha anamaliza kwa kusoma magonjwa ya moyo na njia za kusalimika kutokana na athari zake
Sheikh Ally Nassor
Sheikh Hassan Muhammadyn
Sheikh Shamsi Elmi
Sheikh Muharam Mwaita
Sheikh Salim Qahtwaan
Sheikh Shahid Mohammed
Programu nzito ya kielimu ya elimu za Sharia kwa muda wa mwaka mmoja, ambapo yanakuwa masomo kwa mfumo wa makundi, ambapo makundi ya kimasomo huwa kwa vipindi maalum katika mwaka na kutangazwa kwa njia mbalimbali za mawasiliano na luninga za chaneli za Afrika TV, na usajili wake hufunguliwa kwa muda wa kutosha kabla ya kuanza. Na programu ya stashahada huwa na mihula miwili ambayo mwanafunzi anasoma masomo sita katika kila muhula, na baada ya mwanafunzi kufaulu mitihani ya mwisho kwa mihula miwili, anapata stashahada ya elimu ya Sharia kutoka Africa Academy.
Kozi fupi za Sharia zinazozungumzia mada moja au zaidi katika yale ambayo Muislamu hatakiwi kutokuyajuamiongoni mwa elimu za kisheria. Usajili wa kozi hizo huwa wazi siku zote, ili mwanafunzi aweze kujiunga na kozi hiyo wakati wowote anaotaka na kusoma kwa wakati unaomfaa na kwa kiasi kinachomfaa, na baada ya kumaliza kozi na kufaulu mtihani wake mwanafunzi anapata cheti cha kuhitimu kozi hiyo.
20000
20000
20000
Haki zote zimehifadhiwa © 2023